Kiswahili
 
See also: Habari, HakiElimuRafiki, JosephatNdibalema

We have a Kiswahili chat room at our chat.

Kiswahili material we can publish as FlashDriveContent

If you would like to make more Kiswahili pages, you can create more pages by adding curly brackets { around them like this Jambo.

Kiswahili Wikipedia has more than 5,000 articles. How can we download it?

To copy the Kiswahili Wikipedia - If the copyright notice says that it is okay, then you could use an 'Offline Web Browser' or 'Website Copier' program, such as the free HTTrack program http://www.httrack.com/ to download all of the pages to your hard disk as a collection of linked web-pages. You can then burn it to DVD using a DVD Writer program like Nero Burning ROM or a free equivalent. HTTrack converts the internal HTTP hypertext links between the pages into file links, so you browser from page to page offline. You tell it the top page http://sw.wikipedia.org/wiki/Mwanzo to start at, and it follows the hypertext links on the page to find the other pages, until it has them all. You can do this for any website, if the copyright notice says that it's okay or you have the website owner's permission. ricardo England 18-sep-2007

The Kamusi Project of English-Swahili and Swahili-English dictionaries has a rather liberal copyright policy that seems to allow electronic distribution.

Tamasha la 16 la wiki ya kusoma vitabu nchini Tanzania To: "HakielimuRafiki" <HakielimuRafiki@yahoogroups.com> Ndugu Marafiki, Nimatumaini yangu ya kuwa ni wazima.Ujumbe mbele yenu ni kuhusu tamasha la kusoma vitabu linaloendelea nchini kote nadhani kwa wale mnaofuatilia habari mnajua.Kwa hapa Dar es salaam tamasha hilo linafanyika katika viwanja vya Karimjee toka tarehe 03 mpaka 08 kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni,hakuna kiingilio na wanaoshiriki katika tamasha hilo ni wadau wa sekta ya vitabu nchini kuanzia waandishi,wachapishaji,wauzaji na hata wanunuzi,pia wamekuja na mtizamo mbadala au ufafanuzi wa namna sekta hiyo ilivyo na uhusiano mkubwa na wa moja kwa moja kati ya usomaji vitabu na upunguzaji wa umaskini.

Soma Vitabu Upambane na umaskini ni kauli mbiu ya mwaka huu katika Tamasha la Taifa la Wiki ya Vitabu linalofanyika nchi nzima kuanzia jana.Tamasha hilo limeandaliwa chini ya mwavuli wa Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania [BAMVITA] kwa lengo la kukusisitiza uhamasishaji wananchi wapende kusoma vitabu kwa minajili ya kupata elimu na maarifa yatakayowasaidia kupambana na umaskini.Kwa baadhi ya watu inaweza kuwa vigumu kukubaliana na kauli hiyo kwamba unaweza kuondoa umaskini kwa kusoma vitabu.Kwao hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya dhana ya kusoma vitabu na mikakati ya kuondoa umaskini.

Vitabu ni chanzo kimojawapo muhimu sana kwa upatikanaji wa elimu ya aina yoyote anasema mtunzi mkongwe na Mwenyekiti wa Bamvita,Sharif Adam Sharif. Maendeleo ya taifa lolote yanategemea mikakati mbalimbali endelevu ikiwamo ya kielimu. Hivyo upunguzaji wa umaskini unategemea zaidi kiwango cha ubora wa elimu. Lengo la tamasha ni kutoa mwamko kwa Watanzania kupenda kusoma vitabu,tabia ambayo kwa sasa inaonekana kufa,wanasema waandaaji wanasisitiza kwamba litafanyika katika mikoa 19 kwa wiki nzima kuanzia jana hadi Septemba 8,mwaka huu.

Kwa mkoa wa Dar es salaam tamasha litashirikisha shughuli mbalimbali,Karimjee tamasha linaenda sambamba na maonyesho ya vitabu,hema la watoto linaloshirikisha wanafunzi wa shule za msingi na mashindano ya chemsha bongo kwa shule za sekondari. Nenda ukajionee mwenyewe utajifunza mengi.

Wenu, Mpenda elimu Josephat Ndibalema

Kibaki atabaki kuwa mabaki ya udikteta Africa Mashariki? Uchambuzi na Josephat Ndibalema

KWA baadhi ya watu, tukio la Rais wa Kenya, Mwai Kibaki kufanya hila katika Uchaguzi Mkuu na kusalia Ikulu kwa kipindi kingine cha miaka mitano, linaweza kuonekana la kwanza na la aina yake, lakini ukweli hilo si la kwanza. Hilo ni moja ya matukio ya kawaida barani Afrika na hata duniani kwa wanasiasa kutumia kiinimacho cha uchaguzi kujihalalisha kuendelea kuongoza nchi hata pale ukweli unapodhihiri wameshindwa. Mwaka 1999 katika mkesha wa Krismasi, Mkuu wa jeshi la Wananchi Ivory Coast, Jenerali Robert Guei aliupindua uongozi halali wa Rais Henri Konan Bedie na akaahidi ?kusafisha tu hali ya hewa iruhusu wanasiasa kucheza kwa huru na kidemokrasia?. Yeye binafsi alidai hana nia ya kusalia madarakani muda mrefu. Lakini haikuwa hivyo, akaanza mizengwe katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu aliouitisha mwaka 2000 na yeye akijitangaza kuwa mmoja wa wagombea.

Baada ya kutangaza kuwania urais, Guei aliifumua Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ikaanza kufanya mizengwe ikiwa ni pamoja na kukata majina ya wagombea wawili kati ya watu. Mgombea pekee ambaye jina lake liliachwa ni Laurent Gbagbo. Matarajio ya Jenerali Guei yakayeyuka. Kwanza hatua hiyo iliwaudhi viongozi wengi wa vyama vya upinzani ambao waliamua kuwashawishi wafuasi wao kususia uchaguzi huo. Lakini pili watu wachache waliopiga kura, walimchagua Gbagbo mgombea ambaye kwa macho ya Jenerali Guei alionekana hana madhara.

Hapo Tume ya Uchaguzi ya Jenerali Guei ilipata kigugumizi kutangaza ushindi huo na badala yake Guei akajitangaza mshindi huku akiwaomba wananchi kuwa watulivu. Hatua hiyo ilipokewa kwa maandamano makubwa ya wananchi waliopinga ukiukwaji wa demokrasia na wakafanikiwa Gbagbo akaapishwa kuwa rais.

Maelfu ya waandamanaji wasio na silaha wafuasi wa Gbagbo walijimwaga barabarani kumpinga Jenerali Guei huku wakipambana vilivyo na vikosi vya jeshi vilivyomtetea Guei. Watu zaidi ya 50 waliuawa katika siku mbili za maandamano. Kadri maandamano yalivyopamba moto, baadhi ya vikosi vya polisi viliasi vikaungana na wananchi na vikapanga mapambano makubwa ya silaha dhidi ya vikosi vinavyomuunga mkono Guei.

Mgogoro huo ulifikia kilele baada ya magari manne ya polisi yakiwa yamesheheni askari na bunduki na mizinga kuvamia kituo cha TV jijini Abidjan na kutangaza kwamba wamevishinda vikosi vya Guei. Baada ya hapo vikosi hivyo vilimchukua Gbagbo na kumpeleka kwenye kituo hicho aweze kutangaza kuwa amenyakua madaraka. Kufikia hapo wanajeshi wengi wakabadili mawazo na kuiunga mkono Serikali hiyo mpya na huo ukawa mwisho wa Guei. Ivory Coast kwa muda mrefu ilikuwa inatawaliwa na Rais Felix Houphouet Boigny na baada ya kufariki Henri Konan Bedie ndiye alichukua madaraka hadi alipopinduliwa na Jenerali Guei.

Kwa hiyo matukio ya wananchi wa Kenya kujimwaga mitaani kupinga matokeo yaliyompa ushindi Kibaki wa PNU ni sawa na ilivyotokea Ivory Coast na Yugoslavia ya zamani chini ya Slobodan Milosevic na Kenya. Tabia ya madikteta wote duniani ni kukimbilia haraka kutumia nguvu za jeshi kuwadhibiti watu wanaodai haki yao. Madikteta hao huwa hawajali umwagikaji mkubwa wa damu kutokana na kile wanachodai ni uasi usiovumilika. Nchini Iraq kila ulipoitishwa uchaguzi mkuu wa Rais, Saddam Hussein alikuwa akipata asilimia 100 kwa sababu ya hofu ya mkono wa chuma na aghalabu wapinzani waliuawa mamia kwa mamia. Zanzibar kwa mfano, watu waliokuwa wanapinga matokeo tata yaliyompa ushindi Rais Amani Abeid Karume wa CCM badala ya Maalim Seif Sharrif Hamad wa CUF 'walionja joto ya jiwe' mamia wengine kulazimika kukimbia makazi yao na kwenda Kenya. Nchini Zimbabwe viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani hupigwa kama wahalifu na majeshi ya Serikali wakilazimishwa kukubaliana na hali ilivyo.

Lakini madam kuna mabadiliko ya msimamo kutoka kwa washirika wakuu wa Kibaki, Marekani ambao walikuwa wa kwanza kumpongeza kwa ushindi huo na kwa kuwa nchi takriban zote wahisani zimeyakataa matokeo hayo na kwa kuwa umwagaji damu ni chukizo mbele ya Jumuiya ya Kimataifa atakuwa na wakati mgumu. Wokozi pekee kwake ni kukubaliana na shinikizo la Jumuiya ya Kimataifa kwamba akutane na mpinzani wake anayedaiwa kupokwa ushindi Raila Odinga wa ODM na achote mbinu za CCM za kutengeneza muafaka, kufunika na kuahirisha mara kwa mara kufikia makubaliano.

Ikiwa Kibaki atakaidi mwito wa Jumuiya ya Kimataifa anaweza kufikishwa alipofikishwa Milosevic yaani kushtakiwa na Mahakama ya Kimataifa kwa mauaji ya raia wasio na hatia. Jenerali Guei alitimka Ivory Coast, Saddam alikuja kunyongwa, Robert Mugabe yuko kwenye kikaango. Je, Kibaki atabaki kuwa mabaki ya udikteta Afrika Mashariki

AboutThisPage

Comments

Tue, 18 Mar 2008 06:29:27 UTC wairimo: nyinyi ni wajinga umko africa an mna ongea