Meet with us! Andrius is in Vilnius, Lithuania working on 12Questions.org
Shop with us! SantaMarinella: Completely furnished top flat with splendid views of the sea, Santa Marinella, Italy, from June to October
Wiki with us! 3 hours ago. AndriusKulikauskas: 12Questions/AndriusKulikauskas
Chat with us! 10 hours ago. AndriusKulikauskas: Hi Fred, best wishes to you in your journey to the refugee camps in Uganda.

Karibu RecentChanges SandBox Lists Index Help Preferences Edit

Karibu

Swahili language is spoken by over 100 million people throughout East,Central and parts of Southern Africa.

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa na zaidi ya watu milioni moja, Africa ya Mashariki na Kati, na katika baadhi ya sehemu za kusini mwa Africa

Karibu Katika Wiki ya Kiswahili (Wi-Ki)

Shiriki Katika Juhudi za Kuinusuru Dunia na Athari za MabadilikoYaTabiaNchi

Ukurasa huu wa makaribisho umeandaliwa kukupatia maelezo ya msingi na ya awali kuhusiana na Wavuti hii ya Kiswahili.Mambo yazungumziwayo yanahusu shughuli mbalimbali zikiwemo zakitaaluma pamoja na maelezo mbalimbali yanayohusu uhariri na namna ya kuwasiliana na waongozaji pamoja na washiriki wengine.

Tovuti hii,ijulikayo kama Wiki ya Kiswahili au kwa kifupi, Wi-Ki inaendesha shughuli zake kwa lugha ya Kiswahili kama lugha yake ya kwanza,katika masuala yanayohusu ufundishaji wa lugha ya Kiswahili, upashanaji habari za kimaendeleo, sanaa na utangazaji, kwa ujumla wa lugha na utamaduni wa Kiswahili.

Hata hivyo tunahimiza watumiaji wa lugha hii ya Kiswahili kushiriki katika mjadala mzima wa kukuza Wi-Ki .Wazo hili la kuanzisha Wiki ya Kiswahili bado ni mbegu inayohitaji kukuzwa na wale wote wanaotumia lugha ya Kiswahili. Pia ni vyema kama watumiaji wa lugha hii wataonyesha juhudi katika kutafisiri mawazo na michango yao katika lugha ya Kiswahili kwa faida ya washiriki wengine na hasa watumiaji wakuu wa lugha ya Kiswahili.

Tunawakaribisha wote wenye lengo la kujifunza,kupashana habari, kutangaza na kufundisha lugha ya Kiswahili. Tunakaribisha michango ya mawazo. Tafadhari ungana nasi, jisikie huru hata ka uwezi kuongea na kuandika lugha ya Kiswahili. Mahala hapa utapata fursa ya kujifunza lugha ya Kiswahili na utamaduni unaombatana na lugha husika kwa njia rahisi. Unaweza kujifunza pamoja nasi. KARIBU

Wiki hii ipo chini ya uangalizi wa Wahariri Waongozaji JosephatNdibalema akisaidiana na KiyaviloMsekwa na inafanya kazi chini ya MINCIU SODAS LAB http://www.ms.lt

Karibu katika Nyumba ya Fikira Huru

Mtu mwenye Fikira Huru(fh) kwa lugha ya kiingereza Independent Thinker ni yule mtu anayeweza kutumia uwezo wake aliojaliwa na mwenyezi mungu na kwa kutumia fursa zilizopo anajibidisha ili kujiletea maendeleo yeye mwenyewe pamoja na jamii, mtu mwenye Fikira Huru uweka maslahi ya jamii mbele ili kuleta ustawi katika jamii anamoishi pamoja na yeye mwenyewe. Na hii inatokana na ukweli kuwa binadamu tunaishi kwa kutegemeana, Fikira Huru ubeba thamani ya ubinadamu.Fifira Huru ni Fikira zenye mtizamo wa kijamii zaidi kuliko mtu mmoja mmoja. Dunia ya sasa ni dunia ya ushindani na kwa mantiki hiyo basi kuna haja ya watu wote kufikiri na kushiriki katika shughuli za maendelepo bila kusubiri serikali/mfadhili/shirika/nk, ushiriki wetu wa pamoja katika kujiletea maendeleo utasaidia katika kuyapatia ufumbuzi matatizo yetu ya kila siku.Mahala hapa utaweza kujifunza maswala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo,ubunifu,sanaa na juzi katika kupambanua mambo katika maisha ya kila siku.

Jamii Huru

Watu wenye Fikra Huru ujenga jamii iliyo HURU;

Tunafanya Nini?

Miongoni mwa shughuli zetu kuu ni kuwaunganisha watu toka sehemu mbalimbali duniani tukizingatia mitazamo yao juu ya jamii zinazowazunguka. Minciu Sodas ina zaidi ya washiriki 1000 duniani walio na mitazamo tofauti na wote au baadhi yao tayari wanashiriki ktikaa shughuli za kimaendeleo katika jamii zao. Ungana nasi ili uweze kujifunza zaidi. Na mtu yeyote anawza kushiriki katika kuiendeleza Wiki ya Kiswahili kwa kutoa michango wa mawazo. KARIBUNI

Jifunze Zaidi

Habari zilizijili hivi punde

http://tech.groups.yahoo.com/group/mendenyo/message/2871

Mapendekezo

  • Ebook=Welcome! This is the first page.
  • NextPage=
Karibu changed: November 17, 2009